Fanya Yafuatayo Kama Umeona DALILI za PENZI Lenu Kwenda Mrama

http://chirikumzee.blogspot.com/2015/08/fanya-yafuatayo-kama-umeona-dalili-za.html
Kubali kuwajibika
Japokuwa wengi huwa wanashindwa kwenye kipengele hiki, jibebeshe mzigo wa lawama wewe mwenyewe hata kama si kweli kwamba wewe ndiyo mwenye makosa.

Jiambie mwenyewe kwamba wewe ndiyo umesababisha mfikie hapo mlipofika kwa sababu kama alikukosea, ungeweza kumsamehe kuanzia siku ya kwanza na wala msingefikia hatua hiyo.Ukishakubali kuwajibika, utakuwa kwenye hatua nzuri ya kuzidi kumkaribia, hata ile chuki uliyokuwa nayo, utashangaa inayeyuka kama barafu iyeyukavyo juani na mapenzi yanaanza kuchanua upya moyoni mwako.

Msamehe bure
Kama alikukosea na hajakuomba msamaha, jiambie ndani ya moyo wako kwamba umemsamehe bure na upo tayari kufungua ukurasa mwingine mpya.Lilazimishe tabasamu kwenye uso wake, badala ya kuwa mnapishana kama wanyama, anza kuwa unamtazama usoni kwa upole, hata kama yeye hatakuangalia lakini ataanza kuhisi kitu cha tofauti ambacho kitaanza kumbadilisha naye taratibu.

Rejesha mawasiliano
Mnapokuwa kwenye penzi lililokufa, si ajabu hata salamu mkawa hampeani wala hamzungumzi vizuri tena. Baada ya kuwa umeshayafanya yote niliyokueleza hapo awali, anza kumsemesha.

Msalimu kila mnapoonana, mpigie simu na kumtumia sms nzuri. Hata kama atakuwa hakujibu kwa uchangamfu, usichoke, endelea na taratibu utaanza kuona naye anakusemesha na kukujibu vizuri.Nakuhakikishia kwa mbinu hizi kama penzi lenu lilikuwa limekufa, litafufuka na hata kama mlikuwa mnaelekea nje ya msitari, mtarudi kwenye msitari.
 Mpenzi msomaji wangu, hivi umewahi kuhisi kwamba penzi lako limefikia mwisho japo bado upo na mpenzi wako, mchumba au mumeo/mkeo?
Yaani upoupo tu, zile hisia tamu za mapenzi ulizokuwa nazo wakati mnayaanza mapenzi yenu hazipo tena, hufurahii kuwa naye, hamzungumzi mkaelewana badala yake kila siku ni ugomvi na migogoro isiyoisha!

Kila unachokisema au atakachokisema hata kama ni kizuri vipi kinakuwa sawa na petroli kwenye moto, kinazidi kuchochea uhasama na chuki kati yenu. Kila mnapoanza kuzungumza, hata kama ni jambo zuri lazima muishie kutukanana, kufokeana au kupigana.

Unaishi naye nyumba moja lakini kila mmoja analala kwenye chumba chake, hata mkilala pamoja kila mmoja anageukia upande wake, hujisikii chochote juu yake, hata akiugusa mwili wako unaona kero na hutaki hata kumtazama usoni.

Hujisikii hamu tena ya kuwa naye faragha, kila unachokifikiria kuhusu yeye kinakupandisha hasira na kukuudhi! Unatamani uhusiano wenu ufikie mwisho hata sasa hivi ingawa hujui uanzie wapi.

Ukiona hayo yote niliyoyataja na mengine mengi yanakutokea, huo ni uthibitisho kwamba unaishi kwenye mapenzi yanayoelekea kwenye kifo. Kwa wale ambao wameishi kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa muda mrefu watakuwa wananielewa vizuri zaidi, kama upo kwenye penzi jipya, huwezi kuelewa vizuri.

Kama uko kwenye mazingira ambayo nimeyataja hapo na unaona wazi kwamba penzi lenu siku si nyingi litakwenda mrama, huna haja ya kusubiri na kuacha mwanya penzi life wakati bado mnapendana bali fanya yafuatayo;

jinsi-Mapenzi-ya-kufanya-mapenziSema
hauko tayari kumkosa
Jiwekee nadhiri kutoka ndani ya moyo wako kwamba upo tayari kulifufua penzi lako lililokufa. Jiambie moyoni kwamba utafanya kila kinachowezekana kurudisha furaha, amani, hisia za mapenzi, msisimko na upendo kama ilivyokuwa wakati mnaanzisha uhusiano wenu.

Anza upya
Jipe muda wa kutafakari nini kilisababisha mwanzo mkawa na furaha na kupendana sana. Jaribu kukumbuka mambo uliyokuwa ukimfanyia mwanzo mpaka akakupenda na kuwafanya muishi kwa amani na upendo. Anzia hapohapo, anza kufanya yale yaliyomfanya akupende mwanzo, kuwa mpole kwake, acha kumuonesha kisirani, dharau, jeuri au kujibizana naye. Badili hisia zako za ndani, badala ya kufikiria mabaya yake, fikiria yale mazuri aliyowahi kukufanyia.

Newer Posts Older Posts

© Copyright Chiriku Mzee

Designed By Chiriku Mzee

Blogger Templates

Back To Top