UCHOKOZI! Staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ anatengeneza kichwa cha habari kwa mara nyingine baada ya kudaiwa ‘kujibebisha’ kwa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, kitendo kilichotafsiriwa kuwa ni kumchokonoa mwandani wa jamaa huyo, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’.
Tukio hilo lilijiri usiku mnene Jumapili iliyopita kwenye Ukumbi wa
House Club uliopo Masaki, Dar ambapo kulikuwa na sherehe ya bethdei ya
DJ wa Diamond, Rommy Jones.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu aliyeweka kambi ukumbini humo, Lulu, bila
kujali kwamba, Diamond alimwacha Zari nyumbani akimnyonyesha ‘baby girl’
wao, Latifah Nasibu a.k.a ‘Princess Tiffah’, alionekana akijiachia naye
kimahaba huku akionesha ‘kummisi’ kinoma jamaa huyo.
LIANZA HIVI
Lulu, alikuwa wa mwishomwisho kuingia ukumbini ambapo baada ya kuzunguka
kusalimiana na mastaa wengine alitua kwenye sofa alilokuwa amekaa
Diamond ambapo walianza kufanya yao bila kujali ëwavimba machoí
waliokuwa wakiwakodolea.
Kwa kuwa Diamond alikuwa host (mwendeshaji) wa shughuli hiyo, Lulu
alikuwa akimwaga mauno huku akimshangilia Diamond kufuatia muziki wake
wa nguvu uliokuwa unarindima ukumbini humo.
Kutokana na hali hiyo, Lulu aliendelea kucheza zaidi kwa madai kwamba
anaupenda mno muziki wa Diamond hasa ulipodondoshwa ule wa Mdogomdogo.
WAONESHANA MAHABA
Ilifika wakati Diamond alionekana akimpiga Lulu busu mdomoni huku watu
wakishangilia ëoyoooí lakini wao hawakuwa wakijali chochote kwani
waliendelea kufanya yao.
Kuna wakati walikuwa wakitaniana na kucheka huku wakigongesha glasi zao
za mvinyo na kukumbushana mambo mbalimbali ya siku za nyuma.
Baadhi ya watu walisikika wakisema kwamba, Lulu anamchokonoa mama Tiffah
‘Zari’ kwani kwa usiku huo yeye alikuwa tu nyumbani akinyonyesha wakati
baba mtoto wake akijiachia na kimwana huyo.
“Naona Lulu anatafuta matatizo kwa Zari kwani mahaba wanayooneshana hapa
ukumbini siyo ya kawaida, yaani hawa mastaa wetu mbona majangaaa,”
alisikika mmoja wa wahudhuriaji wa shughuli hiyo iliyokuwa ya kistaa
kwani hakukuwa na ‘watoto wa mbwa’.
SHETTA AMWAGA FEDHA
Katika sherehe hiyo ilipambwa na mastaa kibao wa fani mbalimbali na
mapedeshee wa mjini, walimmwagia Rommy mvua ya fedha huku mwanamuziki,
Nurdin Bilal ‘Shetta’ akimzawadia fedha taslimu Sh. milioni moja ambapo
shughuli iliendelea hadi majogoo.
Wakati hayo yakitendeka mmoja wa marafiki wa karibu wa Zari alimtumia
ujumbe mfupi wa maneno (sms) kumfahamisha juu ya tukio hilo.
MASTAA KIBAO
Ukiacha Lulu na Shetta, baadhi ya mastaa wengine waliojiachia vya
kutosha ni pamoja na Aunt Ezekiel na baba mtoto wake, Moses Iyobo, dada
wa Diamond, Mwajuma Abdul ‘Queen Darleen’, Khaleed Mohamed ‘TID Mnyama’,
Vanessa Mdee ‘Vee Money’ sambamba na Juma Musa ‘Jux’, Hamad Ally
‘Madee’, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ na wengine kibao.
LULU ANASEMAJE?
Akizungumzia hali hiyo, Lulu alisema kuwa ilikuwa ni pati na kupiga
picha na Diamond haikuwa ishu kubwa kwani ni watu wengi waliopiga naye
picha.
“Siamini wala sihisi kama Zari anaweza ‘kumaindi’ ishu kama hiyo. Kama akimaindi atakuwa na lake jambo,” alisema Lulu.
TUJIKUMBUSHE
Kabla ya tukio hilo, Lulu aliwahi kudaiwa kutoka na Diamond lakini
alikanusha vikali ishu hiyo huku akionesha kuwa jamaa huyo hana ubavu wa
kumsogelea wala kufaidi penzi lake.
Chanzo:GPL