DR. SLAA AAMUA KUACHANA NA SIASA RASMI LEO


1.Napenda kumshukuru mwenyezi mungu kwa kutujali uzima.
2. Nimeamua kujitokeza leo hii ili kumesha upotoshaji na kuuweka wazi ukweli.
3.Sina tabia ya kuyumbishwa na ninasimamia ninachokiamini.

4.Sina ugomvi na kiongozi yeyote maana siasa sio uadai.
5. Siasa inapoongozwa kwa misingi ya upotoshaji, matokeo yake ni vurugu.

6. Naweka wazi kuwa mimi sikuwa likizo na hakuna aliyenipa likizo yoyote.

7.Kilichotokea ni kuwa niliamua kuachana na siasa tangu 28.7.2015 saa sita usiku baada ya kutoridhishwa na kilichokuwa kinaendelea ndani ya chama changu.


8.Ni kweli nilishiriki kumleta Lowassa CHADEMA Lakini nilikuwa na misimamo yangu ambayo ilitufanya tusielewane.

9. Baada ya Lowassa kukatwa pale Dodoma, Gwajima ambaye ni mshenga wa Lowassa alinipigia simu kutaka kujua nii cha kufanya.


10. Nilimpigia Mwenyekiti Mbowe kumjulisha na tukakubaliana kupanga muda wa kuwasikiliza.


11. Kabla ya kuanza kuwasikiliza, msimamo wangu ulikuwa ni kumtaka Lowassa kwanza atangaze kuhama chama, aweke wazi ni chama gani anaenda na ajisafishe juu ya tuhuma zake

12.Tangu akatwe jina, Lowassa hakutangaza kujitoa CCM na wala hakujisafisha na tuhuma zake, kitu kilichonifanye nitofautiane naye.

13. Niliwauliza wanachadema wenzangu kuwa Lowassa anakuja kama Mtaji au Mzigo?

14. Swala sio urais kama watu wanavyozusha, mimi nilikuwa nataka mgombea mwenye uwezo na sifa ambaye ataweza kuitoa CCM. Sikuwa na tamaa ya urais kama watu wanavyosema

15. Tangu Gwajima atupe taarifa za ujio wa Lowassa, Swali langu la Lowasssa kuwa Mtaji au mzigo halikuwahi kujibiwa.

16. Nilitaka kujua ni mtaji gani lowassa atakuja nao na ni viongozi gan atakuja nao.

17. Nilijibiwa kuwa anakuja na wabunge 50 wa CCM, wenyeviti 22 wa mikoa na wenyeviti 80 wa wilaya.

18.Baada ya ahadi hiyo, nilitaka sasa nipewe majina ya hawa watu lakini mpaka tarehe 25 july sikupewa hayo majina

19. Wenzangu waliniambia kuwa tarehe 27 niitishe kikao cha dharura ila niligoma kwa sababu nilikuwa sijapewa haya majina
Newer Posts Older Posts

© Copyright Chiriku Mzee

Designed By Chiriku Mzee

Blogger Templates

Back To Top