Najua
nikisema sana nitaonekana kuwa nina mdomo wakati kila kiumbe hapa
duniani kina mdomo, lakini kwa vile kuwapasha ndiyo ‘hobi’ yangu acha
niwachane ‘live’ simuogopi mtu hasa wewe mwenye hila ya kwapa kunuka
bila kidonda.
Mambo mengine unaweza kuona kama ni
kichekesho, kwa vile mimi nyani mzee niliyeishi muda mrefu na kukutana
na shuruba za porini, siwezi kuliacha hivi hivi likapita kwani aibu hii
inashusha heshima ya ndoa.
Siku hizi nyumba ndogo siyo siri tena,
sasa hivi asilimia tisini ya wanandoa lazima wanakuwa na vidumu. Nakuona
mnatazamana na mkeo, ukweli ni huo wewe unayedai wako kwa ajili ya
kukushikia gari ikiwa umechoka uongo?
Wenye ndoa tumekuwa ndiyo hasa tukiwalazimisha waume zetu wazitafute raha nje baada ya ndani kukosekana. Nilielezea wiki jana jinsi wanawake tunaposhindwa kujitambua tukiachika tunasema tumerogwa kumbe wachawi ni sisi wenyewe.
Juzi kuna mwanamke shoga yangu wa karibu
alinieleza kitu kilichonihuzunisha sana. Shoga yangu mwenyewe mwingi wa
habari anawapenda waume za watu ambao anasema wanajua kutunza si waongo
kama masingo. Kama kawaida alimtia mikononi mume wa mtu
aliyejipendekeza. Baada ya kukutana naye alichokutana nacho kilimfanya
amshushe thamani mkewe na kumuona ni mwanamke kimaumbile lakini hana
hulka ya kike.
Anasema baada ya yule mwanaume kukaa
mkao wa kula alichokutana nacho kinatia kichefuchefu. Mwanaume chini
kichaka kimeota unaweza kusuka tatu kichwa, si huko hata makwapani nako
ndiko usiseme mpaka zimebadilika rangi nakuwa za njano. Ikabidi kabla ya
mchezo aingie kazini kumsafisha.
Najiuliza hayo mapenzi na mkewe
wanafanya gizani na hata kama ni gizani, kwa kutumia mkono hawezi kujua
eneo hilo haliko sawa?Kibaya hata aliporudi nyumbani mkewe hakuona
mabadiliko yoyote. Kweli huyo mwanamke kapitia mafunzo ya wanawake
kumjua mwanaume anatakiwa afanyiwe nini?
Siku nilipooneshwa huyo mwanamke mwenye
mume anavyojipenda utashangaa. Yupo smati kila kona ya mwili amechafuka
kwa midhahabu lakini kumtunza mumewe sifuri. Nyumba ndogo imekuwa kubwa
kutokana na kila kitu kinachomhusu mwanaume anakifanya wewe upo tu
unabakia na sifa ya kuolewa lakini unabakia mke jina.
Kwa mtindo huu wanawake wachache
watabakia katika ndoa zao. Jamani hata kwa hili mtasema nachonga sana,
tuliache hivihivi lipite ili umpe nafasi nyumba ndogo.
Hivi kweli wewe mwanamke unamwachia
mumeo na mikucha na minywele kibao hutaki kumnyoa mpaka aende nyumba
ndogo? Aaah! Sipendi miye aibu hii imkute mwanamke mwenzangu, hebu
mtunze mumeo apendeze, huyo anayetaka kukuibia akose kazi ya kufanya.
Hebu basi tunapowafanyia usafi waume
zetu tusiishie kufua tu, bali ni kumfanyia kila kitu kuanzia kucha hadi
kumnyoa kila kona ya mwili wake.Nina imani nimesomeka, ila kama unataka
kutishia mashuzi wakati unaendesha ukichafua hali ya hewa mimi simo
utarudi kijiweni tupige stori.
Ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.