SIASA katika ubora wake! Nyota wa filamu nchini,
Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’ amemchana staa mwenzake, Chuchu Hans
kufuatia kutofautiana kiitikadi kisiasa kati ya chama tawala (CCM) na
Ukawa.
Nyota wa filamu nchini, Jacqueline Walper Massawe ‘Wolper’.
Awali, Chuchu Hans alitangaza kuhamia
Ukawa (Umoja wa Katiba ya Wananchi) na kushiriki kikamilifu kwenye
uzinduzi wa kampeni zao uliofanyika katika Viwanja vya Jangwani, Dar
wiki iliyopita.
BONYEZA HAPA CHINI UCHEKE MPAKA BASS
Lakini ghafla, Chuchu alionekana akiwa
amevaa sare za Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kutangaza kwamba ameamua
kurudi nyumbani, kitendo kilichoonekana kumkera mno Wolper, ambaye
amejipambanua kuwa ni mfuasi namba moja wa mgombea urais wa Chadema,
Edward Lowassa.
“Sijui huu uzalendo wa Tanzania utakuja
lini, yaani wewe juzi tuwe wote na sare uvae, leo umetusaliti kisa
vijisenti sasa aliyekwambia Ukawa tunapewa hela ukaja na mbwembwe zote
nani? Sikuwa na lengo la kukuweka hapa ila nataka niseme kitu kimoja,
jamani hamna kitu kibaya kama unafiki, tamaa na njaa, hii ni nchi yetu
sasa tukihongwa wote ili tuwe chama kimoja ukombozi utakuwa wapi,”
ilisomeka sehemu ya waraka ambao msanii huyo aliuweka katika mtandao
wake wa Instagram.
Chuchu Hans.
Gazeti hili lilimtafuta muigizaji huyo
ambaye ni mpenzi wa Vincent Kigosi ‘Ray’ na alipotakiwa kuzungumzia
jambo hilo, alifunguka:
“Sikutaka kujibu, lakini nimwambie
Wolper ingawa mimi nimewahi kuzaa, lakini yeye ni dada yangu, kanizidi
umri, kwenye siasa kila mtu ana haki ya kupenda kule anakotaka mwenyewe.
Ni kweli nilienda Ukawa, lakini baadaye nikagundua hawana ‘ishu’
nimerudi zangu CCM.”
SOURCE gp